Fiston Mayele jana alifunga bao lake la sita kwenye michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika msimu huu katika ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Marumo Gallants na kuisaidia Yanga kukata tiketi ya fainali ya michuano hiyo
Katika mchezo huo Mayele pia alitengeneza bao la pili la Yanga lililofungwa na Kennedy Musonda. Bao la kwanza la Mayele lilitengenezwa na Musonda na hivyo kufanya pacha ya wawili hao kwenye safu ya ushambuliaji kuwa hatari kwenye shirikisho
Mayele anaendelea kuwania kiatu cha dhahabu katika michuano hiyo akiwa sawa na Ranga Chivaviro wa Marumo Gallants ambaye alifunga bao la kufutia machozi kwa upande wa Marumo jana
Baada ya Marumo kuyaanga mashindano hayo, Ni wazi Mayele yuko kwenye nafasi nzuri ya kuibuka mfungaji bora kwani ana dakika nyingine 180 za fainali kuongeza mabao yake
Mayele ameacha gumzo Afrika Kusini baada ya kuonyesha kiwango bora katika mchezo dhidi ya Marumo
Haikuwa rahisi kwa walinzi wa Marumo kukabiliana nae na kwa hakika walilala na viatu jana

Aidha Mayele na Musonda wameendelea kuwa pacha yenye ufanisi zaidi katika michuano hiyo katika kikosi cha Yanga
Katika mabao sita ambayo Mayele amefunga, mabao matatu yametengenezwa na Musonda ambaye amefikisha assist nne katika michuano ya kombe la Shirikisho. Musonda pia amefunga mabao mawili katika michuano hiyo