Kikosi cha Yanga kilitua mkoani Dodoma jana, leo watakuwa Singida kwa ajili ya kukamilisha maandalizi ya mchezo wa nusu fainali kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) dhidi ya Singida BS ambao utapigwa uwanja wa LITI kesho Jumapili
Yanga inaisaka fainali ya pili msimu huu baada ya kutinga fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika
Nahodha wa Yanga Bakari Nondo Mwamnyeto amesema morali ya wachezaji wote iko juu lengo lao ni kupata ushindi dhidi ya Singida BS na kutinga fainali
TFF imetangaza viingilio vya mchezo huo ambapo VIP ni Tsh 10,000/- na Mzunguuko ni Tsh 5,000/-

Safari ya Yanga kutinga nusu fainali ya michuano hiyo ilikuwa ya kibabe, Wananchi wakiruhusu bao moja tu katika mechi nne ambazo walipachika mabao 20

ADVERTISE HERE