Baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Kagera Sugar jana, Yanga inatarajiwa kushuka kwenye uwanja wa Taifa kuikabili Stand United kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom mzunguuko wa 21.
Kulingana na ratiba iliyotolewa na TFF, mchezo huo unatarajiwa kupigwa kwenye uwanja wa Uhuru, Jumatatu, March 12 2018.
Baada ya mchezo huo Yanga itasafiri kwenda Botswana tayari kwa mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa dhidi ya Township Rollers.
Wakati Yanga wakicheza Jumatatu, wapinzani wao katika mbio za Ubingwa, Simba wao wamepewa 'likizo' wataendelea na michezo ya ligi baada ya mchezo wao wa marudiano kombe la Shirikisho dhidi ya Al Masry.

ADVERTISE HERE