Rais Samia anunua tiketi 5000

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 May 2023
Rais Samia anunua tiketi 5000

Msemaji wa Serikali Gerson Msigwa ameikabidhi Yanga kitita cha Tsh Milioni 20 ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan ikiwa ni bonus baada ya kufunga mabao mawili katika mchezo wa mkondo wa pili nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Marumo Gallants

Tukio hilo limefanyia kwenye Mkutano wa Wanahabari ulioandaliwa na klabu ya Yanga ukifanyika uwanja wa Benjamin Mkapa kuelekea mchezo wa fainali dhidi ya USM Alger ambao utapigwa Jumapili, May 28

Yanga imekusanya jumla ya Tsh Milioni 40 katika hatua ya nusu fainali baada ya kufunga mabao manne kila bao likiwa na bonas ya Tsh Milioni 10

Aidha kuelekea mchezo wa fainali, Rais Dk Samia amenunua tiketi 5,000 kwa ajili ya mashabiki kuingia kwa wingi dimba la Benjamin Mkapa kuisapoti Yanga siku ya Jumapili

Makamu wa Rais wa Yanga Arafat Haji amemshukuru Rais Samia kwa hamasa anayotoa katika michuano hiyo kwani imechangia kwa kiasi kikubwa Yanga kuweza kutinga fainali

Aidha Yanga imemshukuru Rais Dk Samia kwa kutoa usafiri wa ndege itakayowapeleka Algeria kwenye mchezo wa fainali mkondo wa pili ambao utapigwa Juni 03 ambapo ndege hiyo pia itabeba mashabiki

VIINGILIO MCHEZO DHIDI YA USM ALGER

Katika Mkutano huo, Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe alitangaza viingilio vya mchezo dhidi ya USM Alger huku akiwataka mashabiki wa Yanga kuhakikisha wananunua tiketi zote ili kuujaza uwanja wa Benjamin Mkapa

"Tutaanza na tiketi za Royal ambazo ndani yake kumekuwa na package tofauti kama usafiri wa kwenda uwanjani, chakula wakati wa mchezo, jezi maalum za ubingwa wa ligi kuu ambapo kiingilio ni Tsh 200,000/-"

"VIP A ni Tsh 100,000/-, VIP B ni Tsh 30,000/-, VIP C ni Tsh 15,000/- na Mzunguuko ni Tsh 5,000/-"

"Kwa wale watakaokata tiketi za VIP A watakuwa na fursa ya kupata chakula uwanjani kama ilivyo kwa Royal"

"Mchezo utapigwa Jumapili, May 28 saa 10 jioni. Kauli mbiu yetu ni WHY NOT US, TUKUTANE BENJAMIN MKAPA"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’