Mlinda lango wa Yanga Metacha Mnata anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka miwili kuendelea kuwatumikia mabingwa hao wa Tanzania Bara
Metacha alijiunga na Yanga kwa mkopo wa miezi sita akitokea klabu ya Singida BS ambapo mkataba wake na walima alizeti hao unamalizika mwishoni mwa msimu
Baada ya kuonyesha kiwango bora, uongozi wa Yanga umeridhika kumsainisha mkataba wa miaka miwili ambapo sasa msimu ujao ataungana na Djigui Diarra na Aboutwarib Mshery ambaye ameendelea kuimarika majeraha yake
Ni wazi mlinda lango Erick Johora atakuwa huru baada ya mkataba wake kumalizika mwishoni mwa msimu
ADVERTISE HERE