Mlinda lango wa Yanga Ramadhani Kabwili ameelezea kufurahia ushauri aliopewa na kipa mkongwe Juma Kaseja walipokutana kwenye mchezo wa Yanga dhidi ya Kagera Sugar juzi.
Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 lakini baada ya mchezo huo Kabwili na Kaseja walionekana kuteta jambo kwa muda mrefu.
Kabwili amesema kaseja alimpongeza kwa kiwango chake anachokionyesha sasa na kumshauri mambo kadhaa ayafanyie kazi.
Kabwili aliyesajiliwa na Yanga kutoka kikosi cha vijana cha timu ya Taifa, Serengeti Boys, amesema ilikuwa faraja kukutana na mlinda lango huyo mkongwe aliyetamba kwa muda mrefu.
“Kwanza alinipongeza kwa kiwango nilichoonyesha katika mechi dhidi ya Township Rollers licha ya kupoteza mchezo, akanieleza mambo kadhaa ya kurekebisha ili niweze kufikia malengo yangu.
“Alinisisitiza niongezee bidii mazoezini huku nikizidi kuwa na nidhamu lakini pia akanishauri nisiwe na hofu niwapo ndani ya mchezo,†alisema Kabwili.

ADVERTISE HERE