Yanga yafafanua ugawaji wa tiketi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
25 May 2023
Yanga yafafanua ugawaji wa tiketi

Idadi ya tiketi ambazo Yanga imepokea kutoka kwa wadau mbalimbali ni 18,213, uongozi wa Yanga unaandaa utaratibu wa ugawaji wa tiketi hizo

Mkurugenzi wa Wanachama na Mashabiki wa Yanga Haji Mfikirwa amesema kwa sasa wamesitisha zoezi la ugawaji tiketi hizo ili kuandaa utaratibu ambao utawahakikishia waliopewa tiketi wanafika uwanjani

"Tunafahamu baadhi yetu wapo ambao sio waaminifu, wanapopewa tiketi wengine hawaji uwanjani lakini wengine wanaziuza hivyo wale wote wanaotaka tiketi tumewaambia watulie. Tutatangaza utaratibu"

"Lakini pia tunaendelea kupokea tiketi kutoka kwa wadau mbalimbali na kuwahimiza wengine waendelee kununua tiketi ili kuepuka usumbufu wa aina yoyote unaoweza kujitokeza," alisema Mfikirwa

Katika hatua nyingine, Afisa habari wa Yanga Ali Kamwe ametangaza kuwa shamrashamra kuelekea mchezo wa fainali kombe la Shirikisho dhidi ya USM Alger itazinduliwa Ijumaa, Mbagala Zakiem

"Siku ya ijumaa, tutakuwa na Shangwe ya FAINALI ya CAF pale ZAKIEM MBAGALA saa sita mchana. Makundi yetu ya HAMASA ya Yanga yatapaswa kufika eneo hilo. Wadau na watu mashughuli tunawaasa sana wafike eneo hilo. Patawaka moto. Maandalizi ya kwenda KUMKANDA mwarabu," alitamba Kamwe

Jumamosi kutakuwa na jogging ambayo itaanzia Makao Makuu ya Yanga, Jangwani kuanzia saa 12 asubuhi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
1h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
6h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
6h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
10h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’