Wananchi wamejitokeza kwa Zakiem Mbagala katika shangwe la fainali ya kombe la Shirikisho dhidi ya USM Alger, mchezo utakaopigwa Jumapili May 28 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Ni hivi; Wanayanga wako tayari kwa mchezo huu wa kihistoria, ushindi ndio wimbo ambao kila shabiki wa Yanga anauimba
Pamoja na jitihada zinazofanywa na wale wasioitakia mema Yanga kwa kujaribu kuwaondoa Wananchi kwenye 'focus' ya mchezo, hali ni tofauti
Wananchi wameonyesha umoja wakifurahi na kuimba kuelekea mtanange wa kihistoria siku ya Jumapili




ADVERTISE HERE