Kocha Mkuu wa Yanga George Lwandamina ameeleza kutofurahia ratiba ya kikosi chake kinachokabiliwa na mchezo mgumu wa marudiano ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Township Rollers March 17, 2018.
Yanga ilishuka dimbani juzi Ijumaa kuivaa Kagera Sugar na itashuka tena dimbani kesho Jumatatu kuivaa Stand United kabla ya safari ya kwenda Botswana.
Lwandamina amesema anahofia hatapata mda wa kutosha kuwaandaa wachezaji wake kuelekea mchezo huo ambao ni lazima Yanga iibuke na ushindi mnono ugenini ili iweze kufuzu hatua ya makundi.
Aidha amesema hofu nyingine ni majeruhi kwa wachezaji ambao wanacheza michezo mfululizo.
Wakati Yanga ikikabiliwa na ratiba hiyo wapinzani wao kwenye mbio za ubingwa Simba, michezo yao iliahirishwa ili wapate nafasi ya kujiandaa na mchezo wa marudiano kombe la shirikisho dhidi ya Al masry.
Mchezo huo nao utapigwa March 17.
Hii si mara ya kwanza kwa Yanga kukabiliwa na ratiba ngumu msimu huu. Na imeendelea kupata matokeo katika mazingira hayo.

ADVERTISE HERE