Bado kuna utata juu ya usajili wa beki wa pembeni wa Azam FC Gadiel Michael ambaye amemalizana na uongozi tayari kuitumikia Yanga, mabingwa wa kihistoria wa Tanzania.
Azam FC imesisitiza kuwa mkataba wa Gadiel haujamalizika bado na imewaita mezani viongozi wa Yanga kukamilisha taratibu za usajili.
Kauli hiyo imetolewa na Afisa Habari wa timu hiyo Jafar Idd Maganga.
"Gadiel bado ana mkataba na Azam FC. Tunawataka wote wanaomuhitaji basi watume maombi rasmi badala ya kufanya mambo kinyemela," amesema Maganga.
Gadiel yuko kwenye kikosi cha Taifa Stars na amejihakikishia namba ya kudumu kwenye kikosi hicho kinachonolewa na kocha Salum Mayanga tangu mchezaji chaguo la kwanza Mohammed Hussein 'Zimbwe Jr' aumie kabla ya mchezo wa kufuzu AFCON 2019 dhidi ya Lesotho, Juni 10.
Ni miongoni mwa wachezaji walionaswa na Yanga mapema. Azam FC wanadai mkataba wake utamalizika mwaka huu mwezi Disemba.
Bila shaka swala lake litawekwa sawa na uongozi mapema kwani mlinzi huyo ataweza kutoa changamoto sahihi kwa Haji Mwinyi ambaye msimu uliopita alilazimika kucheza karibu kila mchezo baada ya kukosa changamoto kutoka kwa Oscar Joshua.

ADVERTISE HERE