Kwa mashabiki wa Yanga ni masikitiko kuona mchezaji aliyekuwa kipenzi chao anashiriki kutengeneza mgogoro ambao ni wazi dhamira yake ni kuona Yanga inakosa utulivu
Awali madai ya kiungo Feisal Salum kuhitaji kuvunja mkataba na Yanga ilikuwa maslahi lakini leo alipohojiwa na Clouds TV ametaja sababu nyingine, kuwa hana maelewano na Rais wa Yanga Injinia Hersi Said
Akaenda mbali zaidi kwa kusema yeye hana matatizo kabisa na Yanga na kuwa ikitokea Hersi ameondoka Yanga basi atabeba mabegi yake kurejea kambini Avic Town haraka
Katika mahojiano yake pia akamtaja Mdhamini/Mfadhili wa Yanga Ghalib Said Mohammed kuwa alipomtafuta wakati ana matatizo hakupokea simu zake hivyo nae kuamua kutopokea simu pale alipopigiwa na GSM
Ni wazi kwa kile alichozungumza Feisal leo, amedhihirisha kuwa lengo la mgogoro wake sio maslahi bali ni jambo jingine
Uthibitisho wa hayo pia unadhihiri kwa jinsi matukio yake yanavyoandaliwa kila wakati Yanga inapokuwa na mechi au tukio muhimu
Wale ambao wako nyuma ya sakata hili wamedhihirisha kuwa lengo lao ni kuona Hersi na GSM wakiondoka Yanga kwa kuwa wanafahamu watu hawa wawili ndio chachu ya mafanikio ya Yanga katika misimu hii miwili
Ni bahati mbaya kwao kwa sababu Wanayanga wanafahamu thamani ya watu hawa na hawatakuwa tayari kuingia katika mgogoro wowote
Kauli alizotoa Feisal leo zinaweza kufanya viongozi wa Yanga wakaweka msisitizo zaidi katika msimamo wao wa kutaka afuate taratibu ili aweze kuondoka Yanga
Kile alichofanya leo kinaweza kuwa kimefunga kabisa ule mlango wa huruma na kuiacha sheria ichukue mkondo wake