Baada ya kuwa na mchango chanya katika mchezo wa mkondo wa kwanza, Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi huenda akamuongeza dakika za kucheza Bernard Morrison katika mchezo dhidi ya USM Alger hapo kesho
Dakika chache alizocheza katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa, zilikuwa na athari chanya kwa Yanga licha ya Wananchi kukubali kipigo cha mabao 2-1 nyumbani
Bao pekee la Yanga lilifungwa na Fiston Mayele, Morrison aliwahadaa walinzi wa USM Alger kabla ya kumuinulia mpira Mudathir Yahya ambaye alimsetia Mayele
Tangu arejee kutoka kwenye majeraha, Nabi amekuwa amtumia Morrison dakika 15 za mwisho na mara nyingi anapoingia huongeza kasi ya mashambulizi
Morrison alifunga bao la pili la Yanga katika mchezo wa mkondo wa kwanza nusu fainali CAF CC dhidi ya Marumo Gallants
Nabi amebainisha kuwa analazimika kumtumia Morrison kwa dakika chache kwa sababu hana utimamu wa kucheza dakika nyingi