Kiungo mshambuliaji wa Yanga Stephane Aziz Ki amesema wachezaji wote wako tayari kwa mchezo wa mkondo wa pili fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya USM Alger
Mchezo huo utapigwa kesho Jumamosi, Juni 03 katika uwanja July 05 huko Algeria
Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari mapema leo, Aziz Ki alisema wachezaji wamefanya maandalizi ya kucheza mchezo huo wa pili wa fainali hivyo wako tayari
"Kila mmoja yuko tayari, tumefanya maandalizi mazuri kwa ajili ya mchezo huu. Naweza kukuthibitishia kuwa tumesubiri sana mechi hii na sasa imewadia"
"Tutakuwa na mazoezi ya mwisho leo lakini kimsingi wachezaji wote tuko tayari kwa ajili ya kuipambania Yanga," alisema Aziz
Aidha Aziz Ki amesema kuwa wameyasikia maoni ya mashabiki baada ya mchezo wa mkondo wa kwanza uliomalizika kwa Yanga kufungwa mabao 2-1 nyumbani, Aziz ameahidi kuwapa furaha mashabiki wa Yanga siku ya Jumamosi
Majira ya saa 4 usiku kwa saa za Tanzania, Yanga itafanya mazoezi ya mwisho katika uwanja wa July 05 ambao utatumika katika mchezo wa kesho