Msafara wa Yanga ambao unajumuisha mashabiki, wachezaji, benchi la ufundi, viongozi kutoka Yanga, TFF na Serikali (Wizara ya Utamaduni na Michezo), umeondoka Algeria kurejea Tanzania
Msafara uliondoka Algeria saa 7 mchana na wanatarajiwa kuwasili nchini saa 3 usiku
Katika hatua nyingine Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan ameipongeza Yanga kwa kuhitimisha kwa ushindi mchezo wa pili wa fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya USM Alger
"Hongereni sana Yanga kwa hitimisho la mchezo wa Fainali ya Kombe la Shirikisho (CAF Confederation Cup). Historia mliyoandika katika safari yenu ya michuano hii ni kubwa na ya heshima kwa Taifa letu. Nawatakia kheri katika mipango yenu ya siku zijazo," ujumbe wa Rais Dk Samia
Aidha Dk Samia ameandaa hafla maalum ya kuwapongeza Wachezaji wa Yanga itakayofanyika Juni 05, Ikulu jijini Dar es salaam
