Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amesema wako katika hatua za mwisho kukamilisha mazungumzo ya kumuongezea mkataba mpya kocha mkuu wa timu hiyo Nasreddine Nabi
Injinia Hersi amesema mkataba wa Nabi unamalizika mwishoni mwa msimu huu lakini tayari wamechukua hatua mapema ili kuhakikisha anaendelea kubaki Jangwani
"Niwatoe wasiwasi , Nabi yupo sana Yanga . Kila mtu ana mkataba ambao una mwanzo na mwisho, mkataba wake unaisha Msimu huu. Lakini tumeishafanya nae mazungumzo ambayo yapo kwenye hatua za mwisho," alisema Hersi katika mahojiano na Wasafi FM
Aidha akijibu kuhusu tetesi za mshambuliaji Fiston Mayele kuondoka, Hersi amesema Yanga inajivunia Mayele, kuhitajika kwake na timu nyingi ni ishara ya ubora wake na wa klabu ya Yanga kwa ujumla
Amesema jukumu la kwanza ambalo uongozi watafanya ni kumshawishi Mayele aendelee kubaki Yanga lakini kama itashindikana basi watamuuza kwa bei ambayo itakuwa na faida kwa Yanga na kutafuta mbadala mwenye sifa
"Jukumu la kwanza la klabu ni kumshawishi mchezaji bora kuendelea kubaki kama haitawezekana basi tutamuuza kwa bei ambayo ni ina manufaa kwetu na kutafuta mchezaji mbadala wenye sifa kulingana na mahitaji yetu," alisema Hersi