Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze amesema maandalizi kuelekea mchezo wa kuhitimisha msimu dhidi ya Tanzania Prisons yamekamilika, kikosi kikiwa tayari kuwapa furaha mashabiki wao
Kaze amesema kesho ni siku ya kipekee kwa kila Mwanayanga kwani ni siku ya kufurahia mafanikio waliyopata msimu huu
"Kesho ni mchezo wa mwisho wa ligi na ni sikukuu na siku kubwa kwetu ni siku ambayo tunaenda kusherekea mafanikio yetu kwa msimu huu na siku nzuri kuwa na mashabiki wetu"
"Tumekuwa na Safari nyingi na mechi nyingi zenye huzuni na zenye furaha kwetu. Uchovu bado ni mkubwa kutokana na ratiba hii ngumu lakini mara zote tumekuwa tayari kupambana," alisema Kaze
Mchezo dhidi ya Tanzania Prisons utaanza saa 9:30 Alasiri ambapo baada ya mchezo kukamilisha Yanga itakabidhiwa taji la ligi kuu ambalo wamelitwaa kwa msimu wa pili mfululizo
Shamra shamra za ubingwa zitaanza mkoani Mbeya kesho na kuhitimishwa jijini Dar es salaam Jumamosi, Juni 10