Kocha Msaidizi wa Yanga, Cedrick Kaze amesema benchi la ufundi na wachezaji kwa ujumla watapambana kumsaidia straika na kinara wa mabao hadi sasa Ligi Kuu, Fiston Mayele kuhakikisha anafikia malengo yake ya kutwaa tuzo ya kiatu cha mfungaji bora
Kaze amesema hayo leo wakati akizungumza na wandishi wa habari jijini Mbeya wakati akielezea maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo wa kufunga msimu huu 2022/23 dhidi ya Tanzania Prisons
Amesema wanafahamu upinzani ulivyo hadi sasa, hivyo wataangalia kadri ya uwezo wao kumsaidia nyota huyo aliyekosa tuzo hiyo msimu uliopita kutokosa tena heshima hiyo msimu huu
"Tutarajie Mayele ataanza mchezo huo na sisi benchi la ufundi na wachezaji tutapambana kumfanikishia lengo hili aweze kufunga mabao na kutwaa tuzo hii" alisema Kaze
Katika mchezo huo Yanga itawakosa Jesus Moloko mwenye kadi nyekundu, Bernard Morison na Khalid Aucho wenye kadi za njano