Rais wa klabu ya Yanga Injinia Hersi Said amesema kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu kwa misimu miwili mfululizo ni ishara ya Yanga kurejesha ufalme wake katika soka la Tanzania
Msimu huu Yanga imefikia mafanikio ya juu zaidi kwani pamoja na kutwaa taji la Ligi Kuu, Yanga imecheza fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika pia ikiwa imetwaa Ngao ya Jamii
Yanga itacheza fainali ya kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) dhidi ya Azam mchezo utakaopigwa Jumatatu, Juni 12 uwanja wa Mkwakwani
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii Hersi ameandika;
Leo 9th June 2023 katika jiji la Mbeya, @yangasc wametawazwa kuwa mabingwa wa ligi kuu kwa mara 29.
Furaha na fahari kwa klab hii kubwa nchini kurudisha umiliki wa utawala wake katika soka na mataji nchini.
Moja kati ya kipaumbele cha uongozi wetu ilikuwa ni mataji. Taji la pili msimu huu huku tukileta medali za CAF CC.
Inshallah, Azam federation cup iko mikononi mwetu kwa neema za mola wetu.
Nichukue fursa hii kuwapongeza wachezaji wetu chini ya captain wa mataji @mwamnyeto03
pamoja na benchi la ufundi chini ya coach @nabinasreddine
Niwashukuru sana wadhamini wetu wakuu @tzsportpesa media partner wetu @azamtvtz washirika wetu katika bidhaa @gsmgroupofcompanies wahisani wetu @uniceftz na @afya.drinks.tz
Kwenu wananchi, KESHO TUKUTANE KWENYE PAREDI YA TAIFA!!!!