Baada ya shamrashamra za ubingwa wa ligi kuu hapo jana, kikosi cha Yanga leo kinaelekea mkoani Tanga kwa ajili ya mchezo wa fainali kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) dhidi ya Azam Fc
Jumatatu, Juni 12 fainali ya FA itapigwa katika uwanja wa Mkwakwani kuanzia saa 9:30 Alasiri
Hili ni taji la tatu Yanga inawania msimu huu baada ya kushinda Ngao ya Jamii na Ligi Kuu ya NBC
Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema wataondoka Dar majiraya asubuhi kuelekea Tanga ambako jioni watafanya mazoezi yao ya mwisho tayari kwa mchezo huo unaotarajiwa kuwa mkali
Ratiba haijawa rafiki sana kwa Yanga lakini wachezaji wameendelea kupambana na kujitoa ili kutimiza malengo ya timu msimu huu
ADVERTISE HERE