Aliyekuwa kocha wa Yanga Nasreddine Nabi, amewaaga viongozi, wachezaji, Wanachama na Mashabiki wa klabu hiyo akieleza kuwa ni wakati mgumu kwake kuagana na watu aliowapenda sana
Nabi amesema wamekuwa na wakati mzuri katika klabu ya Yanga akipata ushirikiano wa kipekee kutoka kwao
Nabi amewaachia Wananchi ujumbe huu;
"Hili linawezekana kuwa jambo gumu zaidi ambalo nimelazimika kufanya katika miaka miwili iliyopita, lakini mambo yote mazuri lazima yafike mwisho. Tulipitia mihemko yote pamoja, kutoka kwa huzuni hadi furaha, kutoka kwa furaha hadi huzuni, wakati mwingine hasira, lakini kwa neema ya Mungu tuliishi nyakati zisizosahaulika na za kihistoria pamoja"
"Nilipofika hapa, watu wengi walikuwa na mashaka juu yangu, lakini nilikuja na dhamira moja: kuwarudishia furaha na shauku kwa klabu yao kubwa. Haikuwa rahisi hata kidogo lakini matokeo yamekuwa nje ya matarajio yetu"
"Napenda kuwashukuru wachezaji wangu kwa juhudi zao zote, najua wakati mwingine nimekuwa mkali sana kwao lakini jua kwamba ninawapenda kama watoto wangu na kwamba unapompenda mtu, unamtakia mema na ndivyo ilivyotokea"
"Nataka mjue kuwa ninawapenda sana na sitawasahau kamwe. Pia nataka kuwashukuru wafanyakazi wangu wa kiufundi kwa uvumilivu wao na kazi yao yote pamoja nami, kwa sababu bila nyinyi, hili halingewezekana"
"Ningependa pia kuwashukuru wafanyikazi wa Avic Town kwa bidii yao yote; mnafanya kazi bila kuchoka ili kuhakikisha kuwa tuna kila kitu tunachohitaji, hakika ninyi ni watu wa ajabu
"Ningependa pia kumshukuru Bwana Ghalib kwa usaidizi wake wote katika kipindi cha miaka miwili na nusu iliyopita, asante kwa yote ambayo umenifanyia na asante kwa kunitendea kama mtu wa familia yako"
"Napenda pia kuwashukuru viongozi na wajumbe wa kamati ya utendaji. Hatimaye, mashabiki, hakuna maneno yanayoweza kuelezea kiwango cha upendo nilichonacho kwenu na nguvu zote mlizonipa wakati huu"
"Asante sana kwa kila kitu. Naumia moyoni kuachana nanyi, lakini ndivyo maisha ya ukocha yalivyo. Pia ningependa kuwaambia kuwa haijawahi kuwa juu ya pesa, na kwamba muumini mzuri anajua kuwa pesa tunayopata katika maisha yetu tayari imepangwa kwa ajili yetu na kwamba kupata pesa hizo leo au kesho haitabadilisha jambo"
"Mwisho, naitakia kila la kheri klabu yangu ya Young Africans Sc na ninatumai, kwa rehema za Mwenyezi Mungu, kwamba siku nyingine tutakutana tena. Kwaherini familia yangu, nitawakumbuka sana. I love you all Daima mbele nyuma mwiko"