Klabu ya Yanga imesisitiza kuwa mpango wa kwanza ni kumbakisha mshambuliaji Fiston Mayele ambaye anawindwa na timu nyingi ndani na nje ya Afrika
Baada ya Kocha Nasreddine Nabi kuondoka, hofu imetanda miongoni mwa mashabiki wa Yanga wakiwa na wasiwasi kuwa huenda Mayele akafuata
Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amethibitisha kuwa klabu imepokea ofa kutoka timu kadhaa zinazomtaka Mayele lakini ni yeye mwenyewe atakayeamua hatma yake
"Ni kweli tumepokea ofa kutoka timu kadhaa zinazomtaka Mayele lakini kuhusu kuondoka yeye ndio ataamua kwa kuzingatia mapendekezo tutakayompa"
"Mayele bado ana mkataba wa mwaka mmoja, hivyo jambo la kwanza atakaporejea tutampa ofa ya kumuongezea mkataba"
"Kama ataona ofa zilizokuja ni kubwa zaidi, klabu itafanya tathmini juu ya Mkataba wake uliobakia na kuamua thamani yake na baada ya hapo tutakwenda sokoni kusaka mbadala wake," alisema Kamwe
Mayele anahusishwa na klabu kadhaa za Afrika Kusini miongoni ikiwa ni Kaizer Chiefs ambayo Nabi anakwenda kujiunga
Kinara huyo wa kuzifumainai nyavu Ligi Kuu na kombe la Shirikisho barani Afrika 2022/23, pia anawindwa na klabu kutoka Arabuni
Ni wazi haitakuwa rahisi kwa Yanga kumbakisha mshambuliaji huyo tegemeo, ikielezwa tayari mchakato wa kumsaka mbadala wake umeanza