Baada ya kocha Nasreddine Nabi kuondoka, huko mitandaoni na hata katika baadhi ya magazeti zinazotamba ni taarifa za baadhi ya wachezaji kutaka kuondoka
Hili ni kama linafanywa kimkakati ili kuiondolea Yanga utulivu wakati huu viongozi wakiendelea kutafuta kocha mpya
Rais wa Yanga Injinia Hersi Said leo anatarajiwa kuongoza kikao cha Kamati ya Utendaji kufanya tathmini ya msimu uliopita na kuweka mkakati wa msimu ujao
Pamoja na mambo mengine, Kikao hicho kitajadili nafasi iliyoachwa wazi na Nabi ambaye inaelezwa yuko Afrika Kusini kwa ajili ya kujiunga na Kaizer Chiefs
Yanga ina malengo makubwa msimu ujao, hilo litadhihirika siku watakapomtangaza Kocha Mpya na usajili wa wachezaji wapya
Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amewataka Wanachama na mashabiki kuwa watulivu wakati viongozi wao wakiendelea kuweka sawa mikakati