Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amewataka Wanachama na Mashabiki wa Yanga kutoyumbishwa taarifa za upotoshaji zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii na hata magazetini kwani dhamira ya taarifa hizo ni kutaka kuwavuruga
Hersi amesema wanafahamu mafanikio ya Yanga yamewaumiza baadhi ya watu ambao hawakupenda Yanga ifike hapa ilipo
Hersi amewataka Wananchi kuwa watulivu wakati viongozi wao wakisuka mipango, wanajua nini wanafanya ili kuhakikisha Yanga inazidi kusonga mbele
"Sisi viongozi tunajua nini tunafanya licha ya maneno yote ambayo mnayaona kwenye mitandao, magazeti kuhusu sisi Viongozi na kushambuliwa kwa timu yetu"
"Tunajua ni kwa sababu tu ya watu fulani ambao hawapendi kuona Yanga tulipofika kwa sasa. Niwaombe tu kitu kimoja Kutoka kwa wanachama wetu na mashabiki wote wa Yanga, tuendelee kuwa watulivu"
"Wanachama ambao watakaopata nafasi ya kuja kwenye Mkutano Mkuu Jumamosi hii tunawaomba sana waje tuendelee kushirikiana kwa pamoja kuijenga timu hii na kufanya mkutano huu kama katiba yetu ya Yanga inavyotaka tufanye"
"Bado tupo Kwenye mabadiliko na haitoshi bado tunaendelea kuijenga timu kwa gharama yoyote ile ili Yanga iwe imara leo na kesho. Ndugu zangu wanayanga wote nawaomba muwe watulivu muda wetu utapofika kila mtu atafurahi tumejipanga vyema sana," alisema Hersi