Baada ya kumaliza majukumu ya timu ya Taifa, mshambuliaji Fiston Mayele amerejea nchini kuungana na familia yake
Alipotua uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Mayele alipokewa na mkewe ambaye alimkabidhi tuzo za ligi kuu alizoshinda msimu uliomalizika
Wakati tuzo hizo zilipotolewa Juni 12, Mayele alikuwa na kikosi cha DR Congo wakijiandaa na mchezo dhidi ya Gabon
Tuzo alizokabidhiwa ni mchezaji bora wa ligi kuu ya NBC, mfungaji bora na goli bora la msimu pamoja na tuzo ya kuingia kwenye kikosi bora cha msimu
Mayele pia alikuwa mshindi wa tuzo ya mfungaji bora kombe la Shirikisho barani Afrika
Wakati Mayele akitua, aliyekuwa kocha mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi yeye ameondoka nchini leo wawili hao wakikutana uwanja wa Ndege na kupiga picha ya kumbukumbu

