Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema wameanza maandalizi ya mapokezi ya mchezaji mpya ambaye atakabidhiwa jezi namba sita
Kwa takribani misimu minne iliyopita, jezi namba sita ilikuwa ikivaliwa na kiungo Feisal Salum ambaye klabu ya Yanga ilifikia makubaliano ya uhamisho wake kwenda Azam Fc kwa dau la Tsh Milioni 250
Kamwe amesema Yanga imesajili mchezaji wa daraja la juu kabisa ambaye jezi hiyo namba sita atakabidhiwa kwa heshima na taadhima!
Amesema wameanza maandalizi ya mapokezi ya mchezaji huyo ambaye watamtambulisha baada ya utambulisho wa jezi za 2023/24 ambao utafanyika wiki ijayo
"Yanga haitanii, kuna watu wanadhani haya ni masihara, subiri siku hiyo ikifika, hawataamini," alitamba Kamwe
ADVERTISE HERE