Dirisha la usajili tayari limefunguliwa hapo jana na litakuwa wazi hadi August 31, saa 5:59 usiku
Huu ndio wakati mashabiki wa soka wanalazimika kuwa na bando katika simu zao kila siku ili kuhakikisha hawakosi taarifa za usajili kuhusu timu zao
Ni dirisha ambalo mashabiki wa Yanga hawatarajii kuona mabadiliko makubwa katika kikosi chao
Yanga inatarajiwa kuziba mapengo ya maeneo ambayo baadhi ya wachezaji wameondoka baada ya mikataba yao kumalizika
Taarifa za uhakika kutoka ndani ya uongozi wa Yanga zimebainisha kuwa mabingwa hao wa Tanzania Bara wanatarajiwa kusajili wachezaji watano ambao watatu wa kigeni na wawili wa ndani
Baada ya kuachana na Tuisila Kisinda na Bernard Morrison, Yanga ina nafasi mbili za nyota wa kigeni huku ikwa bado kuna nyota mwingine wa kigeni atapewa mkono wa kwaheri
Kwa wachezaji wa ndani, mpaka sasa Yanga imetangaza kuachana na wachezaji watatu ambao ni Dickson Ambundo, Abdallah Shaibu na Erick Johora