Wachezaji wa Yanga leo wataripoti kambini Avic Town tayari kwa safari ya Malawi ambako Julai 06 watacheza mechi ya Kimataifa ya kirafiki dhidi ya Nyasa Big Bullets katika Maadhimisho ya Uhuru wa Malawi
Yanga imealikwa na Serikali ya Malawi kwenda kupamba sherehe za Uhuru wa nchi hiyo. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan atakuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo
Wananchi leo wako makini wakisubiri taarifa ya utambulisho wa moja ya wachezaji waliosajiliwa katika dirisha hili la usajili ambaye atajumuishwa katika safari hiyo
Jana Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe aliwaambia Waandishi wa Habari kwa heshima ya mwaliko huo, Rais wa Yanga Injinia Hersi Said ametoa zawadi kwa Wananchi wa Malawi kumshuhudia mmoja wa wachezaji mahiri aliyesajiliwa katika dirisha hili ambaye atasafiri na timu
Yanga ilipanga kutambulisha usajili wake baada utambulisho wa jezi, tukio ambalo limepangwa kufanyika wiki hii
Utambulisho wa leo ni maalum na pekee kwa ajili ya heshima waliyopewa Yanga na Serikali ya Malawi
Je atakuwa nani? ndio swali ambalo Wananchi wanajiuliza, majibu yatapatikana baadae
Hatakuwa yule namba sita ambaye Kamwe anamtangaza kila siku kwani huyo atakuwa wa mwisho kutambulishwa
Yawezekana mchezaji atakayetambulishwa leo ni mzawa, kwani haitarajiwi nyota wa kigeni akaweza kufika kwa wakati kuwahi safari hiyo
Utaratibu wa msimu uliopita nyota wapya walikuwa wakitambulishwa kuanzia saa sita usiku lakini huyu wa leo huenda akatambulishwa mapema kwani jioni anapaswa kuwa Avic Town na wenzake