Mbunifu wa jezi za Yanga Sheria Ngowi amesema matoleo matatu ya jezi msimu wa 2023/24 kila moja ina maana yake
Jezi ya kijani ambayo ndio ya nyumbani inabeba historia ya klabu ya Yanga ambayo imetimiza miaka 88. Jezi hiyo ina michoro ya 88 iliyowekwa kwa mtindo wa maua

Jezi ya njano ambayo ni ya ugenini ubunifu wake umebeba heshima ya Yanga kucheza mechi nyingi pasipo kupoteza msimu uliopita. Ngowi amesema ubunifu wake umechagizwa na ule mchezo maarufu wa simu wa kupanga matofali. Kocha Nasreddine Nabi aliiwezesha Yanga kucheza mechi 49 mfululizo pasipo kupoteza

Jezi ya tatu ambayo ni nyeusi/blue imeonyesha michoro 88 yenye nyota kati ikibeba mafanikio ya Yanga msimu uliopita. Jezi hiyo chini ina ufito wenye mfano wa medali ambazo Yanga wametwaa msimu uliopita
