Utambulisho wa wachezaji unadhaminiwa na CRDB

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
12 Jul 2023
Utambulisho wa wachezaji unadhaminiwa na CRDB

Baada ya utambulisho wa Nickson Kibabage, ikapita wiki nzima pasipo Yanga kutambulisha mchezaji mwingine kabla ya jana kumshusha beki kisiki Gift Fred

Presha ilikuwa juu miongoni mwa mashabiki na Wanachama wa Yanga ambao baadhi yao walianza kuamini yale yaliyokuwa yakiandikwa mitandaoni

Utambulisho wa Gift leo umedhaminiwa na benki ya CRDB na umetoa majibu kwa nini Yanga ilichelewa kutoa taarifa za usajili wake

Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amefafanua kuwa ulikuwa mkakati wa kibiashara ambao umeifanya Yanga kuwa klabu ya kwanza kuwa utambulisho wa wachezaji wake wapya kudhaminiwa (pesa imeingia klabuni)

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Kamwe ametoa ufafanuzi huu

"Kwanini Yanga imechelewa kutambulisha wachezaji? Swali jepesi kutoka mtaani na baadae ikawa Topic nzito kwenye vyombo vya Habari.

Waandishi wakaandika. Wachambuzi wakazungumza. Presha ikapanda kwenye mioyo ya mashabiki na baadhi wakaanza kuamini kwenye ‘Uzushi’.

Mara Yanga imefungiwa kusajili.. Mara viongozi hawana hela .. Blaah Blaah zikawa nyingi.

Lakini leo, kupitia utambulisho wa GIFT FRED MAJIBU YAMEPATIKANA.

Utambulisho wa wachezaji ni Content yenye Thamani kubwa sana. Uhitaji wake hufanya watu kukesha, kukopa fedha kulipia/kutafuta habari sahihi inapopatikana.

This Time YANGA tukasema Hapana. Let’s Try kitu kipya. Thamani hii tuigeuze kuwa Fedha kwa Klabu yetu.

Ni kama ambavyo wachambuzi husema, wachezaji flani flani Ulaya usajili wao ulilipa siku ya kwanza baada ya kutambulishwa.. Kwanini Hilo lisifanyike hapa Tanzania?

Kwa Msisimko huu wa Football ya Tanzania kwenye mitandao ya Kijamii, kwanini hii isiwe sehemu ya pato la klabu?

Idara za wachapakazi wa Yanga SC zikaingia kazini. Demand ikatengenezwa sokoni, miswada ikaandaliwa na kusambazwa kwenye Makampuni na hatimaye, BENKI YA CRDB wakabeba Package hii ya Udhamini wa utambulisho wa Wachezaji wetu Msimu huu.

Football ni Biashara Mabibi na Mabwana.. Na Uongozi huu wa Yanga chini ya Rais Hersi Said unataka kushinda uwanjani na kushinda kwenye akaunti zetu za Benki

Mambo mazuri zaidi Yanakuja Wananchi"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
1m ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
3h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
8h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
8h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
12h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’