Makocha wa Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
12 Jul 2023
Makocha wa Yanga

Unaambiwa baada ya Miguel Gamondi kupewa mkataba wa kuinoa Yanga haraka akawaagiza mabosi wa mabingwa hao wa nchi kuhakikisha wanamnasa Kocha Moussa Ndao raia wa Senegal

Awali Yanga ilikuwa kwenye mazungumzo na kumrejesha aliyekuwa Kocha Msaizidi Cedric Kaze kabla ya mapendekezo ya Gamondi kuzima mpango huo

Gamondi amewahi kufanya kazi na Ndao katika klabu ya Wydad Athletic hivyo anamfahamu vizuri

Ndao amecheza Wydad na kuifundisha timu hiyo katika vipindi tofauti tofauti. Ni nadra sasa kocha mweusi kuaminiwa katika hizi nchi za kiarabu, ni lazima awe na kitu cha kipekee

Akiwa mchezaji Ndao amecheza Morocco, Algeria, Misri na UAE katika klabu ya Al Hilal

Katika majukumu yake ya ukocha, Ndao amedumu katika benchi la ufundi la Wydad kwa vipindi vitatu tofauti na kushinda mataji yote ya ndani, Ligi ya mabingwa na CAF Super Cup

Huyu ni kocha mwenye uzoefu mkubwa na soka la Kaskazini, uzoefu huo anauleta Yanga kwa kushirikiana na Gamondi ambaye pia ni mzoefu wa soka la Kaskazini

Yanga ina mkakati wa kufanya vizuri katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika msimu huu, hawa ni makocha walioletwa kuifanya kazi hiyo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’