Tujitokeze kufanya shughuli za kijamii - Arafat

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Jul 2023
Tujitokeze kufanya shughuli za kijamii - Arafat

Makamu wa Rais wa Yanga Arafat Haji amewataka Wanachama na Mashabiki wa mabingwa hao wa nchi kushiriki matukio ya kurudisha kwenye Jamii katika kipindi hiki cha Wiki ya Mwananchi

Umekuwa sehemu ya utamaduni wa Yanga kufanya shughuli mbalimbali za kijamii kuelekea kilele cha Wiki ya Mwananchi ambapo mwaka itakuwa Julai 22 uwanja wa Benjamin Mkapa Yanga ikitarajiwa kucheza mechi ya Kimataifa ya kirafiki dhidi ya Kaize Chiefs

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Arafat ameandika ujumbe huu;

"Wiki hii tumetangaza kuzindua rasmi #WikiYaMwananchi2023 ambayo kilele chake kitakuwa siku ya Jumamosi ya Julai 22, 2023 pale kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Kupitia Wiki ya Mwananchi, klabu yetu huwa inafanya shughuli mbalimbali za kijamii, hivyo basi tunaomba wananchi wote nchi nzima tuungane katika kushiriki shughuli za kijamii ambazo zitaainishwa na klabu.

Kila mmoja katika eneo lake anaweza kushiriki shughuli mbalimabli za kijamii ambazo tutawatangazia siku tutakapozindua rasmi Wiki ya Mwananchi na shughuli au mambo ambayo tumelenga kufanya kwa mwaka huu.

Zaidi ya yote, nitumie fursa hii kuwaalika wananchi wote tujitokeze Uwanja wa Benjamin Mkapa siku ya kilele cha Wiki ya Mwanachi Julai 22, 2023 tujumuike kwa pamoja kabla ya kuuanza msimu wa mashindano 2023|24.

Kutakuwa na burudani siku nzima kuanzia utambulisho wa wachezaji wetu wote, burudani za wasanii wakali wa muziki, mechi ya kirafiki dhidi ya Kaizer Chiefs timu kubwa na kongwe Afrika Kusini na Afrika kwa ujumla lakini pia kutakuwa na surprises za kila aina.

Mwananchi mwenzangu usipange kukosa kuwa sehemu ya historia ya kilele cha #WikiYaMwananchi2023. Kwa mara nyingine tena tunataka kuithibitishia Afrika na dunia sisi ndio timu kongwe zaidi na yenye mashabiki wengi Tanzania kwa kuujaza uwanja!

NB: Pichani ni 11+6 wa Siku ya Mwananchi"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’