Bakari Nondo Mwamnyeto 'Kapteni Beka'

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Jul 2023
Bakari Nondo Mwamnyeto 'Kapteni Beka'

Ameandika Afisa Habari wa zamani wa Yanga Hassan Bumbuli

Hadi sasa hakuna mchezaji mzawa aliyetingisha usajili kwenye dirisha hili kwa.maana ya kuzigonganisha timu kubwa tatu za juu katika kuwania saini yake

Mara ya mwisho kushuhudia miamba ya soka Tanzania Yanga, Simba na Azam FC ikipigana vikumbo kwa kuwania saini ya mchezaji wa ndani kwa nguvu kabisa ni msimu wa 2020/2021 na mwamba aliyeigonganisha ni huyu Mdigo, Bakari Nondo Mwamnyeto

Aliingia Yanga ikiwa chini ya nahodha Lamine Moro, hakukuwa na nahodha msaidizi baada ya Juma Abdul kuondoka, hivyo aliyekuwa kocha Msaidizi, Juma Mwambusi na Meneja, Hafidh Saleh walipendekeza jina la Mwamnyeto kuwa Nahodha Msaidizi na alipata kura 16 kati ya 19 za wachezaji

Akawa nahodha wa kuchaguliwa kidemokrasia. Kiwango cha Lamine kiliyumba, Mwamnyeto akaanza kuvaa kitambaa cha Unahodha 'Usinga' na hata Yanga walipoachana na Lamine tayari usinga wa Yanga ulishamzoea

Akiwa nahodha ameingoza Yanga kutwaa mataji sita kwenye misimu miwili na pia kufika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika

Pamoja na mafanikio ya uwanjani Mwamnyeto anabaki kuwa mchezaji ghali Mtanzania ambaye alitingisha dirisha la usajili Tanzania

Usajili wake Jangwani, ulikutana na maandiko hasi kutoka kwa baadhi ya waandishi na wachambuzi wanaoaminika kuwa na nguvu hapa nchini. Kuna waliodiriki kusema alipaswa kwenda nje ya nchi na si Yanga na kuna waliosema anakwenda kupotea mbele ya Lamine na wengine walimtabiria anguko kubwa la kurejea Coastal Union msimu unaofuata

Uteuzi wake kuwa nahodha msaidizi ulihojiwa na utaratibu uliotumika ulizua gumzo kwenye vyombo vya habari na kila kitu cha Mwamnyeto kikawa stori kubwa

Kuna wakati hakuwa sawa, maneno yakawa mengi, na wengi walidhani ndio mwisho wake huku watesi wake wakipata upenyo kutaka kumalizia, lakini alijipanga upya na kurejea kwa nguvu, kasi na maarifa zaidi kuliongoza jahazi la Wanajangwani

Ahsante nahodha, ahsante kapten wa viwango unayetoa somo nzuri kwa wachezaji wenzako wazawa bila kushika chaki

Mwamnyeto ana nidhamu, heshima, upendo na utu, zaidi ameshika dini. Mwamnyeto una msemo wako 'Kila hatua Dua.' Usiache kumuomba Mwenyezi Mungu katika kila hatua unayoipitia

Kila la heri katika msimu mpya!

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
6h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
14h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
17h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
20h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’