Mjumbe wa kamati ya utendaji na Katibu wa Kamati ya Mashindano Yanga Samuel Lukumay amesema kambi ya kikosi cha Yanga nchini Botswana inaendelea vizuri kila kitu kipo sawa na wachezaji wote waliosafiri na timu wako salama kwa ajili ya mchezo wa kesho dhidi ya Township Rollers.
“Maandalizi yanaendelea vizuri hatukupata shida yoyote tangu tunakuja hadi tumefika, tulitembelewa na balozi wa Tanzania nchini Afrika kusini ambaye ndio anasimamia pia Botswana akapata muda wa kuzungumza na vijana na kuwatia hamasa na kuwaambia katika mpira kila kitu kinawezekana kwa hiyo tunaweza kugeuza matokeo.â€
“Hakuna majeruhi yoyote kiujumla kambi inaendelea vizuri bila tatizo loloteâ€
Mchezo wa awali uliozikutanisha Yanga na Township Rollers kwenye uwanja wa Taifa, yanga ilipoteza kwa kufungwa 2-1 hivyo inahitaji kushinda kuanzia 2-0 ili kukata tiketi ya moja kwa moja kufuzu hatua ya makundi ya vilabu bingwa Afrika.

ADVERTISE HERE