Mchezo wa kilele cha wiki ya Mwananchi kati ya Yanga dhidi ya Kaizer Chiefs umemalizika kwa furaha upande wa Wananchi baada ya Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0
Kennedy Musonda alifunga bao pekee la Yanga kwenye dakika ya 45 akimalizia pasi murua kutoka kwa Max Mpia Nzengeli
Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi alitumia vikosi viwili, kipindi cha pili akibadili wachezaji 10 alioanza nao
Yanga ilikuwa bora na pengine Wananchi walistahili kuibuka na ushindi mnono leo
Nyota wapya Skudu Makudubela, Max, Jonas Mkude, Yao Yao, Gift Fred wote walikuwa na mchezo mzuri leo
Kwa hakika huu ni mwanzo mzuri kwa vijana wa Gamondi





ADVERTISE HERE