Kuna Jonas Mkude, fundi wa kupiga pasi zenye anuani! Yawezekana Mkude ndio mchezaji mahiri zaidi katika ligi ya Tanzania Bara kwa uwezo wake mkubwa wa kupiga pasi kutoka upande mmoja wa uwanja kwenda mwingine
Jana katika mchezo dhidi ya Kaizer Chiefs, Mkude aliwapa Wananchi burudani kwa dakika 45 ambazo zilitosha kumtambulisha timu ya Wananchi
Kuna Mudathir Yahya ambaye baada ya kufanya vyema msimu uliopita katika kikosi cha Nasreddine Nabi, sasa amekomaa

Uwezo wake wa kutumika katika nafasi zaidi ya moja uwanjani unamfanya awe mchezaji wa kipekee
Pia kuna Salum Abubakar 'Sureboy' ambaye dakika chache alizopewa jana ziliwahakikishia Wananchi kuwa watarajie kupata kile alichofanya misimu iliyopita
Halafu kuna Zawadi Mauya, huyu Mauya aliyecheza mechi ya Kaizer Chiefs alikuwa fundi sana!

Kuna watu hawaamini huyu ni Mauya au ni yule Sergio Buesquets aliyekuwa Fc Barcelona? Maana isije kuwa ameondoka Hispania akawa amekuja Tanzania badala ya Marekani kama ilivyotangazwa!
Kuna Khalid Aucho ambaye msimu uliopita alikuwa 'engine' ya Nabi katika kikosi chake. Bila shaka hata kwa Gamondi Aucho ataendelea kuwa mchezaji muhimu
Itoshe kusema Yanga ina utajiri mkubwa wa wachezaji katika eneo la kiungo, nani atacheza itategemea na mahitaji ya kimbinu ya Gamondi kulingana na mechi