Tuko tayari kwa mchezo - Mwandila

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
17 Mar 2018
Tuko tayari kwa mchezo - Mwandila
Township Rollers na Yanga kila moja anaingia katika mchezo wa leo Jumamosi utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Botswana akiwa na lengo la kufuzu kwa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Akizungumza katika mkutano na wanahabari jijini Gaborone, kocha msaidizi wa Yanga, Noel Mwandila ‪alisema kikosi chake kipo tayari kuivaa Rollers, hasa baada ya kupata ushindi katika mechi zake za ligi ya nyumbani.

“Baada ya mechi ya Rollers tumecheza mechi mbili katika Ligi Kuu Tanzania na zote tumeshinda mabao matatu kila mechi, kwa hiyo tunaamini ushindi huo umetuongezea kujiamini zaidi.

“Tuna wachezaji wetu wawili hawatakuwepo katika mchezo uliopita, lakini habari njema ni kurejea kwa nahodha wetu ambaye hakuwepo katika mchezo uliopita, atakuwepo kesho,” amesema Mwandila

Naye kocha wa Rollers, Nikola Kavazovic alionyesha umuhmu wa mechi hiyo kwa historia ya soka la Botswana kama wakifanikiwa kusonga mbele watakuwa timu ya kwanza ya nchi hiyo kuingia hatua ya makundi.

“Kwa sasa tunatambulika katika timu 20 bora Afrika, tulianza kwa kuwatoa Al-Merreikh na kuonyesha kiwango cha juu katika mchezo wa kwanza uliochezwa Tanzania. Naamini tunastahili kusonga mbele na tutafanya kazi kutimiza hilo.

Yanga ni timu kubwa Afrika na sisi ni timu inayokuwa, lakini tunaamini sasa sisi tunapewa nafasi kubwa ya kusonga mbele,” alisema Kavazovic.

“Najivunia wachezaji wangu, lolote litakalotokea kesho Jumamosi, tumefanya mambo makubwa kuliko ilivyotegemewa katika mechi zote zilizopita.

“Bao la pili tulilofunga katika mchezo wa kwanza dhidi ya Yanga, limeonyesha aina ya uwezo wetu. Bao lile ubora wake ni zaidi ya viwango vya Afrika… ni bao la kiwango cha dunia, tulipiga pasi 21 ndani ya dakika moja na sekunde 40 bila ya wachezaji wa Yanga kugusa mpira hadi tumefunga bao. Tutaendelea kucheza kwa mtindo huo hata kesho,” alisema Kavazovic.

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
1h ago
READ MORE →
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
4h ago
READ MORE →
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
9h ago
READ MORE →
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
9h ago
READ MORE →
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
9h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
13h ago
READ MORE →
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE →
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE →
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE →
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE →