Kiungo mshambuliaji wa Yanga Mahlatse Makudebela maarufu Skudu amesema licha ya ushindi mkali kwenye kiwanja cha mazoezi, atapambana kuhakikisha anapata nafasi ya kucheza
Skudu alikabidhiwa jezi iliyopambwa zaidi katika dirisha hili la usajili, jezi namba 6 hivyo anafahamu ukubwa wa majukumu aliyonayo
Nyota huyo raia wa Afrika Kusini, amesema ni furaha kwake kujiunga na timu kubwa yenye wachezaji bora na zaidi mashabiki wenye upendo
"Nafurahi kwa mapokezi na upendo mkubwa walionionyesha mashabiki. Niko hapa kupambana ili kuwapa furaha"
"Nikuhakikishie, tuna timu bora. Ni kazi kubwa kupata namba hapa kwani wachezaji wengi wako vizuri na wote wanahitaji nafasi ya kucheza hivyo mtihani mkubwa ni kuonyesha uwezo utakaonifanya kucheza kwenye kila mchezo"
"Naheshimu ubora wa wengine kwani najua tumekuja kwa ajili ya kuipa timu mafanikio na kitakachotupa nguvu ni ushirikiano na juhudi binafsi, lakini nafahamu kuwa natakiwa kuonyesha juhudi za hali ya juu kama nataka kucheza," alisema Skudu
Katika mchezo wa kilele cha wiki ya Mwananchi dhidi ya Kaizer Chiefs, Skudu alianza kwenye kilichotumika kipindi cha kwanza na alikuwa hatari zaidi akitokea winga ya upande wa kushoto