Kiungo Gael Bigirimana ameonekana akishiriki mazoezi ya kikosi cha Yanga Avic Town
Imeelezwa kuwa Bigirimana amepewa ruhusa kushiriki mazoezi akijiweka fiti kwa ajili ya msimu ujao
Bigirimana alikuwa sehemu ya kikosi cha Yanga msimu uliopita, aliondoka katika usajili wa dirisha dogo nafasi yake ikichukuliwa na Mamadou Doumbia ambaye hata hivyo nae amepewa 'Thank You'
Sio jambo geni kwa mchezaji kuruhusiwa kufanya mazoezi na timu aliyowahi kuitumikia
Yanga ina nafasi moja ya nyota wa kigeni, wakitarajiwa kusajili mshambuliaji atakayechukua nafasi ya Fiston Mayele
Katika mahojiano na chombo kimoja cha habari, Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe alisema kabla ya dirisha la usajili CAF kufungwa, watamtangaza mshambuliaji waliyemsajili
ADVERTISE HERE