Kikosi cha Yanga kimehitimisha wiki ya pili ya mazoezi ya pre-season Avic Town
Benchi la ufundi chini ya Kocha Miguel Gamondi wanaendelea kuwaandaa vijana kwa ajili ya msimu mwingine wa makombe
Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema furaha imetawala Avic Town ambako Yanga imeweka kambi yake ya pre-season
"Mpaka sasa benchi la ufundi linaendelea na program za mazoezi Avic Town, taarifa za pre-season tunazitoa kupitia Yanga TV nafikiri wengi wanafuatilia"
"Furaha imetawala Avic Town, wachezaji wanafanya mazoezi huku wanaburudika. Msimu huu tutawafunga watu mabao na pia tutatoa burudani kwa mashabiki wetu," alisema Kamwe
Aidha Kamwe amethibitisha kuwa wikiendi hii Yanga inatarajiwa kucheza mechi moja ya kirafiki yakiwa ni mapendekezo ya benchi la ufundi