Baada ya kuwapagawisha Wananchi katika mchezo wa kilele cha Wiki ya Mwananchi dhidi ya Kaizer Chiefs wiki iliyopita, mshambuliaji Crispine Ngushi amesema Wanayanga watarajie makubwa zaidi kutoka kwake
Tangu aliposajiliwa na Yanga dirisha dogo msimu wa 2021/22, Ngushi aliandamwa na majeraha ya mara kwa mara ambayo yalimfanya asipate nafasi kwenye kikosi cha kwanza
Ngushi amepona majeraha hayo na sasa yuko fit na tayari kuwapa Wananchi kile walichotarajia kutoka kwake
"Najiandaa vema na msimu ujao ili kuwapa wanayanga kile ambacho wanakitegemea kutoka kwangu. Msimu uliopita sikufanya vizuri kwani nilikumbwa na majeraha yaliyonifanya kukosa nafasi hivyo muda mwingi niliutumia kujiweka sawa ili nianze msimu ujao nikiwa kamili"
"Nawaahidi wanayanga kuwa msimu ujao nitawaonesha kile kilichofanya nikasajiliwa na klabu hii kubwa Tanzania na Afrika. Naitaka namba na nitahakikisha najituma ili kocha anipe nafasi niweze kutoa mchango wangu Kwa timu yangu," alisema Ngushi
Kama ataendeleza kile alichofanya dakika 45 alizocheza katika mchezo dhidi ya Kaizer Chiefs, ni wazi Ngushi atakuwa na nafasi kwenye kikosi cha Gamondi