Kampuni ya Jackson Group ambayo ilipewa dhamana ya kuithaminisha Yanga, imekamilisha mchakato huo
Hatua inayofuata ni Yanga kutangaza thamani yake na kuwakaribisha Wawekezaji kununua asilimia 49 za hisa kulingana na Katiba ya Yanga
Hiyo ni hatua ya mwisho katika kukamilisha mchakato wa Mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa klabu ya Yanga
Nini kinakwenda kutokea?
- Yanga itaendelea kubaki chini ya Mkutano Mkuu General assembly) , Baraza la wadhamini, wajumbe wa kamati ya utendaji na wanachama
- Yanga itafungua KAMPUNI ambayo yenyewe itamiliki 51% za hisa zote na kuwaachia wawekezaji 49% za hisa zilizobaki
- Kampuni hii mpya kazi yake itakuwa ni kuendesha shughuli za mpira na BIASHARA za mpira pekee kwa niaba ya Yanga
- Kampuni hiyo itakuwa na uongozi wake ambao ni BODI ya WAKURUGENZI ambao watamuajiri mtendaji mkuu (CEO) ambaye yeye naye ataajiri watendaji wote chini yake wakumsaidia kuendesha hii kampuni kama TAASISI ya mpira.
- Kwenye bodi ya wakurugenzi itakayoanzishwa kusimamia kampuni hiyo kutakuwa na jumla ya wajumbe (9) wa bodi, Yanga SC itatoa wajumbe (5) na WAWEKEZAJI kwa UJUMLA wao watatoa wajumbe (4)
- Nafasi moja ya ujumbe kwenye bodi itapatikana kwa kununua (12.5%) ya hisa, hivyo ili muwekezaji apate nafasi kwenye bodi lazima anunue angalau asilimia hizo za hisa kuingia kwenye bodi
- Katiba ya Yanga imeelekeza ni lazima kuwe na wawekezaji zaidi ya mmoja watakaonunua 49% ya hisa na wasiozidi wanne
ADVERTISE HERE