Mshambuliaji wa Yanga Hafiz Konkoni amesema anafahamu matarajio ya mashabiki kwake ni makubwa lakini anahitaji angalau wiki mbili za mazoezi aweze kuwa fit
Konkoni ametua Yanga akitokea klabu ya Benchem United ya Ghana. Usajili wake ulikamilishwa baada ya Yanga kumuuza aliyekuwa mshambuliaji kiongozi Fiston Mayele kwenda klabu ya Pyramids Fc
"Nafahamu mashabiki hapa wana shauku kubwa kwangu hasa baada ya kuondoka Mayele (Fiston), nawahakikishia nitapambana ili niweze kuwapa furaha"
"Nimepata nafasi ya kuitwa timu ya Taifa ya Ghana, nitapenda niendelee kuwa katika kikosi cha timu ya Taifa hivyo najua nina kazi ya kufanya"
"Nawaomba mashabiki wanipe muda ili niweze kuwa tayari, ligi ya Ghana ilimalizika tangu mwezi Juni, nimekuta hapa wenzangu wameanza mazoezi, nitahitaji angalau wiki mbili ili niweze kuwa katika utimamu," alisema Konkoni