Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi atakuwa na kazi ya kuamua kikosi chake cha kwanza kutokana na ushindani ambao wachezaji wote wameonyesha katika kiwanja cha mazoezi
Djigui Diarra, Metacha Mnata na Aboutwalib Mshery wote walipata nafasi katika mechi za kirafiki na kuonyesha umahiri wao
Diarra anaweza kuwa na uhakika zaidi kwa sababu ya uwezo wake wa kutumika kama 'sweeper keeper'
Walinzi wa pembeni vita ni kali Kibwana Shomari, Yao, Joyce Lomalisa na Nickson Kibabage wote wameonyesha wako tayari
Safu ya ulinzi wa kati ni hatari tupu nahodha Bakari Nondo Mwamnyeto, Dickson Job, Ibrahim Hamad 'Bacca' na Gift Fred
Hapa kwenye safu ya ulinzi Gamondi anaweza hata akaamua kurusha shilingi kuchagua nani wa kuanza nae kwani wote ni 'wamoto'
Eneo la kiungo cha ulinzi Khalid Aucho, Jonas Mkude, Mudathir Yahya na Zawadi Mauya wote wako tayari kutumika huku Salum Abubakar, Farid Mussa, Pacome Zouzoua na Stephane Aziz Ki nao wakiwa tayari katika eneo la viungo washambuliaji
Crispine Ngushi amezaliwa upya! ameuwasha sana moto kwenye uwanja wa mazoezi pengine Wananchi wasishangae wakimuona katika kikosi cha Gamondi
Maxi Nzengeli ni kiraka katika eneo la ushambuliaji ametumia kama kiungo mshambuliaji na winga, ameonekana kumudu majukumu yote
Skudu winga ya kushoto ni kama amejimilikisha wakati Denis Nkane akionyesha anataka kuwamo kwenye kikosi cha kwanza huku Jesus Moloko akiendeleza pale alipoishia msimu uliopita
Kennedy Musonda anaweza kushuhudiwa akianza kwenye safu ya ushambuliaji wakati Hafiz Konkoni akiendelea kutengeneza 'fitness' akiwa amechelewa kujiunga na wenzake
Unaweza kusema Gamondi ana vikosi viwili, anaweza kuanza na kikosi chochote na timu yake ikapata matokeo mazuri