Anaandika Meneja wa Digitali klabu ya Yanga, Privaldinho;
Ukitazama trailer ya Documentary au cover utaona picha ya viongozi wakuu Injinia Hersi Said na Arafat Haji
Kwanini? Kwanza hawa ndio wabeba maono ya historia hii. Eng Hersi wakati anaingia Yanga mtakumbuka alisema tusipobeba makombe niulizeni mimi
Watu wengi walimkejeli baada ya msimu uliofuta kukwama. Katika nyakati za masimango na kebehi hakuyumbishwa
Msimu uliofuata akaenda DR Congo akarudi na Mayele, akamleta Diarra. Akafanya usajili mzito.
Wakasema amefungua kikundi cha band ya Wakongo. Uzuri ile band ikatumbuiza vyema. Akamshawishi GSM atoe zaidi ya milion 200 za mabadiliko
Kimsingi alifanya risk kubwa sana kumshawishi boss wake kuwa nipe Bilion 2 tuwalete laliga tubadili mfumo, ipo siku mambo yataka sawa
Akamshawishi GSM apeleke timu AVIC na kusajili baadhi ya wachezaji pamoja na kusaipoti klabu kiuchumi. Unadhani ilikuwa jambo dogo?
Ukifuatilia documentary ya Madrid ya Leyenda Blanca kwenye cover yupo Florentino Perez, kwa sababu ndiye mbeba maono
Ukitizama dokumentari ya Failure and success of galacticos era trailer yake kwa sekunde takriban 45 imepambwa na Perez. Kwanini kwa sababu yeye ndiye mbeba maono
Katika historia ya mpira wa Tanzania, Hersi anaweza kuwa Rais wa klabu mwenye mafanikio makubwa na mfano wa kuigwa na mwenye uthubutu wa kipekee kwenye historia ya vilabu vyetu
Makombe sita, medali ya CAF, pamoja kufanikisha mchakato wa mabadiliko sio jambo dogo. Ukimtazama Hersi ni kama anajaribu kupita njia za mogul wa soka la AFRIKA kama Irvin Khoza ambaye akiwa na miaka 43 aliichukua Orlando Pirates mwaka 1991 na hatimaye mwaka 1995 akabeba ubingwa wa CAF
Utakumbuka hivi majuzi wakati tunawapiga Mazembe kwao, Moise Katumbi alipiga makofi mbele ya Hersi, haikuwa jambo dogo
Siamini kama miaka kumi iliyopita kama Eng aliwahi kufikiria ipo siku tukio kama hilo litatokea. Utakumbuka Katumbi nae aliichukua Mazembe akiwa na miaka 33 pekee akiwa na ndoto za kupasua anga la kimataifa
Baada ya miaka 11 Katumbi akavaa medali ya CAF. Hersi ndani ya mwaka mmoja tayari amevaa medal ya CAF. Dokumentari yetu imebeba maono