Mwamnyeto awaalika Wananchi Mkwakwani

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 Aug 2023
Mwamnyeto awaalika Wananchi Mkwakwani

Nahodha wa Yanga Bakari Nondo Mwamnyeto amewaalika Wananchi wajitokeze kwa wingi uwanja wa Mkwakwani leo katiika mchezo wa nusu fainali ya Ngao ya Jamii dhidi ya Azam Fc

Kwa mara nyingine Mwamnyeto anaiongoza Yanga katika uwanja wa Mkwakwani dhidi ya Azam Fc ikiwa ni miezi miwili imepita tangu aliponyanyua taji la FA katika uwanja huo

"Sisi tumejiandaa vizuri, tuko tayari kwa mchezo huu wa nusu fainali Ngao ya Jamii. Nawaomba mashabiki wetu waje kwa wingi kuishangilia timu yao"

"Tuna wachezaji wapya wamesajiliwa hii ni nafasi yao kuja kuwaona na pia kutushangilia katika mchezo huu ambao tunahitaji kushinda"

"Tunajua haitakuwa mechi rahisi kwa sababu tumeshinda Ngao ya Jamii mara mbili, tunasaka kwa mara ya tatu, lakini tumejiandaa na tutahakikisha tunapata ushindi siku ya leo ili tuingie fainali," alisema Mwamnyeto

Nae Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema kikosi chake kiko tayari kwa mchezo huo ambao wanatarajia utakuwa mgumu

"Tunafuraha kuwa hapa, tumefanya maandalizi mazuri, wachezaji morali yao iko juu, wameonyesha kuwa tayari kwa mchezo huu"

"Utakuwa mchezo mzuri kwa sababu utatuonyesha tuko wapi sasa, mkakati wetu ni kusaka ushindi huku tukicheza soka safi"

Viingilio vya mchezo huo VIP B ni Tsh 30,000/- na Mzunguuko ni Tsh 10,000/-

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
8h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
13h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’