Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi jana aliwatumia nyota wapya watatu katika kikosi kilichoanza kwenye mchezo wa nusu fainali ya Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC
Mchezo huo uliopigwa uwanja wa Mkwakwani, uliwashuhudia Wananchi wakitinga fainali kibabe kwa ushindi wa mabao 2-0. Huo ulikuwa ushindi wa tano kwa Yanga dhidi ya Azam Fc katika mechi sita zilizopita
Katika kikosi chake Gamondi alianza na Maxi Mpia Nzengeli, Skudu Makudubela na Yao Kouassi. Skudu alitoka baada ya kupata majeraha kwenye dakika ya 7 nafasi yake ikichukuliwa na Crispine Ngushi ambaye pia alitoka dakika ya 65 nafasi yake akimpisha Clement Mzize
Kama utatoa alama kwa kila mchezaji katika mchezo huo, Yao na Maxi ni miongoni mwa wachezaji waliopata alama za juu katika kikosi cha Yanga

Maxi alitawala eneo la kiungo ambalo alikuwa akibadilishana majukumu ya Farid Mussa aliyetoka baadae nafasi yake kuchukuliwa na Stephane Aziz Ki
Bila ya mpira Maxi aliongoza katika 'pressing' na kuwapa wakati mgumu walinzi wa Azam Fc ambao walijikuta wakifanya makosa mengi pamoja na mlinda lango wao
Bao la kwanza lililofungwa kwa ufundi wa hali ya juu na Aziz Ki, pasi ilitoka kwa Maxi. Bao la pili pia ambalo alifunga Mzize, Maxi alihusika kwa kuwatia msukosuko walinzi wa Azam Fc ikawa rahisi kwa Mzize kupora mpira na kuuweka kambani
Jana Wananchi walimsahau rasmi Djuma Shabani baada ya kushuhudia kiwango bora kutoka kwa Yao
Yao alizuia kwa ustadi mkubwa lakini alipandisha mashambulizi kwa kasi. Ukizungumzia wachezaji wenye 'mapafu ya mbwa' basi ni aina hii
Utamuona katika eneo la winga wakati timu inashambulia na pia utamuona kwenye safu ya ulinzi wakati timu inazuia
Kwa hakika huu ni msimu mwingine unaokuja na mafanikio, kuna dalili ya Documentary nyingine msimu ujao...!