Timu ya Wanawake ya Yanga Princess imeanza rasmi kambi yake ya Maandalizi jana Agosti 9-2023 Jijini Dar es Salaam Kwa ajili ya msimu mpya wa ligi kuu ya Wanawake Tanzania Bara 2023-24 inayotaraji kuanza mwezi ujao
Meneja wa Yanga Princess Mata Gwasa amesema maandalizi yameanza vyema huku Wachezaji wote wameripoti wakiwa na Afya njema na hakuna majeruhi yoyote mpaka sasa
"Tumefanya Usajili wa kutosha kwa kuingiza wachezaji wengi wenyewe uzoefu na wenyewe vipaji hivyo timu zingine zitarajie ushindani mkubwa kutoka kwetu" alisema Gwasa
Aidha Gwasa amepongeza ukuaji wa soka la wanawake hapa nchini na kusisitiza soka la Wanawake litaleta mafanikio makubwa kwa nchi
"Kwasasa tumepiga hatua katika soka la wanawake na mafaniko ambayo tunayapata katika Ligi yetu ndiyo yanapelekea tunakuwa na timu za Taifa za wanawake zenye wachezaji wenyewe vipaji ambao wanapambana na kutuletea makombe nchinia"