Gamondi alia na safu ya ushambuliaji

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Aug 2023
Gamondi alia na safu ya ushambuliaji

Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amewaomba radhi mashabiki wa timu hiyo baada ya kushindwa kutetea Ngao ya Jamii kwa msimu wa tatu mfululizo

Jana Yanga ilipoteza kwa mikwaju ya penati mchezo wa fainali dhidi ya Simba baada ya matokeo ya suluhu ya bila kufungana ndani ya dakika 90

Gamondi amesema walistahili kushinda mchezo huo kwani walicheza vizuri kuliko wapinzani wao lakini walikosa umakini katika eneo la umaliziaji

"Nawaomba radhi mashabiki kwa kupoteza mchezo huu kwenye penati, tulistahili kushinda. Kipindi cha kwanza tulicheza vizuri na kutengeneza nafasi lakini hatukuzitumia. Kipindi cha pili tulikuwa bora zaidi, sikumbuku kama wapinzani wetu walitengeneza nafasi yoyote ya wazi, hatukupata ushindi kwa sababu hatukufunga bao lakini tulicheza vizuri sana"

"Hili ni somo kwetu, tunarudi kwenye kiwanja cha mazoezi kufanyia kazi mapungufu hayo lakini kwa ujumla nimefurahishwa na jinsi wachezaji wamecheza katika dakika zote za mchezo," alisema Gamondi

Katika mchezo huo Yanga ilitwala kila idara, Jesus Moloko na Musonda walifunga mabao lakini yote yalikataliwa kwa sababu walikuwa katika eneo la kuotea

Yanga inarudi kujiandaa na mchezo wa hatua ya awali ligi ya mabingwa dhidi ya ASAS Fc ambao utapigwa Jumapili ijayo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
2h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
12h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
19h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’