Jambo pekee ambalo linawaumiza mashabiki wa Yanga ni kuona timu yao imeshindwa kutetea Ngao ya Jamii kwa msimu wa tatu mfululizo baada ya kupoteza kwa mikwaju ya penati mchezo wa fainali dhidi ya Simba
Yanga ilikuwa na kila sababu ya kumaliza mchezo huo mapema, bahati haikuwa upande wao tu
Lakini jambo moja la uhakika ni kuwa mechi dhidi ya Simba jana imezika mjadala juu ya ipi timu bora kwa sasa Tanzania
Ni hivi; kama kuna timu itamaliza ligi kuu msimu huu ikiwa na alama nyingi kuliko Yanga, basi itatwaa ubingwa
Wakati wa usajili kulikuwa na tambo nyingi lakini sasa tambo hizo hazisikiki, wanafahamu ushindi wao wa Ngao ya Jamii ni bahati pamoja na makosa ya kibinadamu ya waamuzi
Mbele ya Yanga jana Simba haikuonyesha maajabu yoyote, hili liko wazi
Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi ameanza vyema majukumu yake, amehakikisha analinda ubora wa timu iliyoachwa na Nasreddine Nabi na kuimarisha zaidi
Kwa soka ambalo Yanga wameonyesha mkoani Tanga, ni wazi kikosi cha Gamondi kiko tayari kufanya makubwa zaidi msimu huu