Mshambuliaji Simon Msuva anayechezea Difaa El Jadida ya Morocco ameisaidia timu hiyo kutinga hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika baada ya kupata sare ya mabao 2-2 dhidi ya AS Vita huko DRC.
Difaa imefuzu kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-2 baada ya kushinda kwa bao 1-0 katika mchezo wa kwanza uliopigwa nchini Morocco ambapo Msuva alifunga bao hilo.
"Asante Mungu kwa nafasi nyingine sasa ni hatua ya makundi Dua zenu. Nadhani ni wakati Mzuri wa mimi Kukua na kosegea Ehh Mungu nisaidie," ameandika Msuva katika ukurasa wake wa mtandao wa Instagram.
Tangu ajiunge na Difaa El Jadida akitokea Yanga mwaka jana, Msuva amekuwa mmoja wa wachezaji wa kutegemewa wa timu hiyo.
Tayari ameifungia mabao 13 katika mashindano yote.
Kushiriki hatua ya makundi ya michuano hiyo mikubwa kabisa barani Afrika kutamfanya aonekane zaidi na pengine kutimiza ndoto za kwenda kucheza barani Ulaya

ADVERTISE HERE